Header

Jackie Chan kumsikiliza Chris Tucker kuhusu muendelezo wa ‘Rush Hour’

Muigizaji maarufu Chan Kong-sangJackie Chan’ amethibitisha kuwa muendelezo wa filamu ya yake na Chris Tucker ‘Rush Hour’ Sehemu ya 4, utaanza kutengenezwa mapema mwakani(2018).

Akizungumza na The Cruz Show ya Power 106 FM ya nchini Marekani Jackie Chan amethibitisha taarifa hizo alipokuwa akitambulisha filamu yake mpya inayokwenda kwa jina ‘The Foreigner’ ambapo ameongeza kuwa itafanyika iwapo muigizaji mwenzake Chris Tucker atakubali.

Jackie Chan na Chris Tucker

Ni miaka isiyopungua 10 sasa tangu Jackie Chan na Chris Tucker wameungana katika kuanzisha na kuendeleza mfululizo wa filamu hii ya ‘Rush Hour’.

Itazame tailer rasmi ya filamu ya Jackie Chan ‘The Foreigner’.

Yasikilize mahojiano ya Jackie Chan kupitia

Comments

comments

You may also like ...