Header

Chege Chigunda ndani ya mwaka mwingine na Bruno Mars pamoja na Nick Cannon

Aliyeufatilia muziki wa Bongo Fleva Tanzania, kuanzia miaka ya 2000 ni hakika anamfahamu vyema kimuziki Mkongwe ‘Chege Chigunda’ kwa ushiriki na uzalishaji wa ladha tamu ya burudani ya muziki na kikubwa kuwa Chege hajakatika kusikika masikioni mwa wapenda burudani mpaka sasa na kulithibitisha hilo ni kupitia kazi yake mpya sokoni ambayo inaonekana kuendelea kufanya vizuri’ iite ‘Runtown’.

Moja ya vitu vya kipekee vilivyo ndani ya ubarikiwa wa Chege Chigunda ni upekee wa sauti yake nyenye uzito wa wastani ambayo mara nyingi mashabiki wa muziki wake ukutana nayo kwa asilimia kubwa katika ladha ya muziki iliyo katikati ya uimbaji na uchanji(Rap Sing).

Chege Chigunda

Miaka kadhaa iliyopita, tarehe 8 Octoba alizaliwa Chege na kila mwaka tarehe kama hii uikumbuka kama siku pekee ya kuzaliwa kwake. Uzuri wa siku kama hii katika kumbukumbu ya kuzaliwa, Chege amezaliwa katika siku ya mfanano wa tarehe na Staa wa muziki ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Grammy kutoka Marekani Bruno Mars na mwaka huu anatimiza umri wa miaka 31.

Bruno Mars

Siku hii pia sio tu kwa mhususi ya kumbukumbu kwa Chege na Bruno Mars, bado ni kumbukumbu ya mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Staa wa Marekani, Muigizaji, Rapa, Mchekeshaji, Muongozaji wa Filamu, Mtangazaji na mjasiriamali Nicholas Scott “Nick” Cannon na kwa mwaka huu anatizima umri wa miaka 36.

Nick Cannon

Staa Nick, ni wazi kuwa hayuko tena katika huba na mpenzi wake Mariah Carey mahusiano yaliyovunjika mwaka huu wa 2017 ambapo katika kumbukumbu ya jambo la aina yake katika kuikaribisha siu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, mwaka 2014 Nick aliweka wazi kuwa ameifunika tatoo ya jina la aliyekuwa mpenzi wake Mariah Carey kwa mchoro mpya wa tatoo ya ishara ya Yesu kuwekwa msalabani.

Kwa wote wanaosherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa miaka kadhaa iliyo pia tarehe ya leo, Dizzim Online inawatakiwa maisha marefu na yenye baraka tele.

Comments

comments

You may also like ...