Header

Tammy The Baddest na Jay Moe uso kwa uso kwa nguvu ya Chapaa

Rapa wa kike kutoka Tanzania anayefanya poa na kazi yake aliyomshirikisha Mkongwe Juma Mchopanga ‘Jay Moe’, Tammy The Baddest ameachia rasmi video ya ngoma yake ya ‘Chapaa’ ikiwa ni kazi mpya chini ya uongozwaji wa Director Joowzey.

‘Chapaa’ ikiwa ni ngoma nyingine baada ya ‘Mtoto wa Kike’, mara hii ni kazi iliyoandaliwa ndani ya ushirikiano wa watayarishaji wawili ambao ni ‘Chizain Brain na Bugaleez kutoka katika Studio za B Records.

Mpaka sasa miongoni mwa wasanii wanaopanda kwa kasi zaidi na wamepata nafasi ya kufanya kazi na mkongwe wa muziki, rapa Jay Moe ni Tammy The Baddest kiasi ambacho yalizuka maneno maneno ya kutilia mashaka ukaribu wao mpaka wao kufanya kolabo ya ngoma yao ya ‘Chapaa’ kitu ambacho Jay Moe akinusha uwepo wa mahusiano nje ya kazi za muziki kati yao.

Comments

comments

You may also like ...