Header

ZaiiD asifia ‘Wowowo’ kwa ushirikiano wa Couple ya Bongo Movie

Mkali wa muziki wa rap kutoka Tanzania, Zaiid baada ya ngoma yake ya ‘Umeme Umerudi’ amedondosha kazi yake mpya inayo kwenda kwa jina la ‘Wowowo’ ngoma iliyoingia katika masikio ya mashabiki wengi wa kiume na kuwaacha wakilengwa lengwa na udenda kwa kuvutia wazo picha la kinachozungumzwa katika wimbo.

Zaiid ili kukata kiu ya wote waliotamani kuona nini kitaandaliwa kwa ajili yao katika muonekano wa picha/video alimpa jukumu hilo muongozaji wa video za muziki ‘Inno Mafuru’ ambapo zoezi la uchukuaji picha lilifanyika katika mikoa miwili ya Tanzania, Arusha na Dar Es Salaam.

Katika ‘Wowowo’ kingine kilichoipamba zaidi video hiyo ni kuonekana kwa couple ya Leo Mysterio na Staa wa maigizo kutoka katika kiwanda cha filamu za kitanzania(Bongo Movie), Riyama Ally aliyecheza baadhi ya vipande vyenye burudani ya haina yake vinavyoleta maana halisi ya maudhui ya wazo la wimbo.

Comments

comments

You may also like ...