Header

Magoli ya Salah Misri yamkumbusha Drogba Ivory Cost ya 2006

Mchezaji wa zamani wa Chelsea pamoja na timu ya Taifa ya Ivory Cost Didier Drogba ameonyesha kuvutiwa na kiwango alichoonyesha Mohamed Salah katika Mchezo dhidi ya Congpo DR baada ya kuisaidia Misri kukata tiketi ya kucheza kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Mohamed Salah ambaye ni Mchezaji wa Klabu ya Soka ya Liverpool ameipeleka timu yake ya Taifa ya Misri katika Fainali hizo zitakazofanyika nchini Urusi ikiwa ni mara kwanza kwa timu hiyo kwa kipindi cha miaka 28 huku Salah, 25 akifunga magoli mawili dakika ya 63 pamoja na lile la penati dakika ya 95 ya Mchezo baada ya mwamuzi kuamuru penati katika Mchezo huo dhidi ya Congo DR ambao ulikua muhimu kwa Misri kushinda ili kukata tiketi ya Michuano hiyo yenye hamasa kubwa Duniani itakayofanyika Mwakani.

Kupitia ukurasa wake wake wa mtandao wa kijamii wa twitter Drogba ameweka ujumbe wa kumpongeza Salah huku akimkumbushia Mwaka 2006 wakati wa Kombe la Dunia nchini Ujerumani kwenye Kundi C timu ya Ivory Cost ikimaliza nyuma ya Argentina pamoja na Uholanzi.

Misri inaungana na Mataifa 13 ambayo tayari yamefuzu huku ikiwa ni nchi ya pili kufuzu kwa bara la Afrika baada ya Timu ya Taifa ya Nigeria kukata tiketi tayari.

Comments

comments

You may also like ...