
Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, Davido amepatwa na msiba mwingine baada ya ule wa mshikaji wake ‘Tagbo’ aliyekutwa kauwawa na kutelekezwa kando ya hospitali, tukio ambalo liliibua utata kiasi cha Davido kuhusishwa katika uchunguzi wa kujua nini chanzo cha kufariki kwake.

DJ Olu
Kupitia ukurasa wake wa Snap Chat Davido alituma ujumbe wa masikitiko ya kumpoteza Dj wake na rafiki yake kipenzi DJ Olu ambaye ni mtoto wa mfanyabiashara maarufu wa mafuta nchini Nigeria na mwanakikundi cha HKN ambaye amekutwa amekufa katika gari lake siku ya Jumamosi, Oktoba 7.

Davido aliandika kupitia Mstandao wa Snap Chat

Maneno ya Davido juu ya Msiba wa Dj wake ‘DJ Olu’
Hata hili ni tukio lingine la msiba kumuangukia Staa wa Nigeria Davido, ikiwa wiki iliyopita alipatwa na msiba wa mshikaji wake wa karibu Tagbo, na mpaka sasa inawezekana kuwa Davido yuko katika orodha ya watakaoisaidia polisi kubaini nini kilimkuta Tagbo.
Comments
-
Chege Chigunda ndani ya mwaka mwingine na Bruno Mars pamoja na Nick Cannon
-
Magoli ya Salah Misri yamkumbusha Drogba Ivory Cost ya 2006