Header

Hallelujah ya Diamond x Morgan Heritage yakamata #1 BBC 1Xtra

Ngoma ya Diamond Platnumz ‘Hallelujah’ aliowashirikisha nguli wa muziki wa reggae toka Jamaica, Morgan Heritage, imekamata nafasi ya kwanza kwenye Top 5 ya kipindi cha Destination Africa cha BBC Radio 1Xtra.

Diamond ameandika kwenye Instagram,” Number One in United Kingdom (UK), #Hallelujah ft @morganheritage….Thank you so Much @bbc1xtra @iamdjedu and all the fans for the Major support…. Africa to the World! full Video link in my BIO.”

Nao Morgan Heritage wameandika,” No 1 in the #UK is a blessing. ‪Our brother @iamdjedu @1Xtra thanx for the support on our new song #Hallelujah by @diamondplatnumz ft @morganheritage.”

Video ya wimbo huo hadi sasa ina views milioni 3.8.

Comments

comments

You may also like ...