Header

Baada ya kuikosa nafasi kombe la Dunia, Robben atangaza maamuzi yake aliyofikia

Aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Uholanzi ambaye anakipiga katika klabu ya Bayern Munich Arjen Robben ametangaza kustaafu kuchezea timu ya Taifa mara baada ya timu yake Kushindwa kufuzu kucheza Fainali za kombe la Dunia mwakani.

Robben, 33 ambaye alifunga magoli yote mawili katika Mchezo wa mwisho wa kufuzu kucheza kombe la Dunia siku ya jana dhidi ya timu ya Taifa ya Sweeden amesema uamuzi huo ni mgumu kwake lakini umri umemtupa mkono na anahitaji kuelekeza nguvu zake katika Klabu yake.

Licha ya kuibuka na Ushindi dhidi ya Sweeden Uholanzi imeshindwa kukata tiketi ya kushiriki michuano hiyo huku Ufaransa ikikata tiketi ya moja kwa moja kushiriki Michuano hiyo itakayofanyika Mwakani nchini Urusi.

Arjen Robben alianza kuichezea timu ya Taifa mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 23 amefunga magoli 37 mpaka sasa akiwa ni Mchezaji namba nne kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote kwa Taifa hilo.

Comments

comments

You may also like ...