Header

Baada ya Robben kutangaza kustaafu timu ya taifa, nyota mwingine wa Bayern afata nyayo

29 AGOSTO 2015 / LEVERKUSEN Arturo Vidal en partido valido por la BendesLiga 2015-2016, entre Bayern Leverkusen vs Bayern Munich, partido jugado en el estadio BayArena FOTO CORDONPRESS / AGENCIAUNO

Baada ya timu ya Taifa ya Chile kushindwa kufuzu kucheza kombe la Dunia mwaka 2018 kiungo wa timu hiyo Artudo Vidal anayekipiga katika klabu ya Bayern Munich ametangaza kustaafu kuchezea timu ya Taifa.

Vidal, 30 ambaye anakipiga katika Klabu ya Bayern Munich amefikia uamuzi huo ikiwa ni muda mfupi tangu timu yake ya Taifa ifungwe na Brazil magoli 3-0 ukiwa ni Mchezo wa mwisho wa kusaka tiketi ya michuano ya kombe la Dunia huku Brazil ikiwanyima nafasi Chile ambao wamemaliza nafasi ya sita katika Kundi lao.

Vidal ni miongoni mwa Wachezaji walioipa mafanikio makubwa timu ya Taifa ya Chile ikiwemo kuisaidia timu hiyo kushinda ubingwa wa Copa America mara mbili Mfululizo mwaka 2015 na 2016.

Comments

comments

You may also like ...