Header

Diamond Platnumz yulee.. afanya video na Rick Ross

Diamond Platnumz anazidi kupaa kimataifa.. Ikiwa ni wiki kadhaa tu tangu aachie video ya wimbo wake na Morgan Heritage, Hallelujah, amefanikiwa kushoot video ya wimbo aliomshirikisha rapper wa Marekani, Rick Ross. Chibu anakuwa msanii wa pili Afrika kuwahi kumshirikisha bosi huyo wa Maybach Music Group, baada ya P-Square.

Video hiyo imefanyika jijini Miami, Florida na muongozaji akiwa ni Mr Moe Musa.

Meneja wa Diamond, Babutale amepost picha hiyo juu na kuandika: Kuthubutu ni sehemu ya kufanya. Dhamira yetu ni kuupeleka mziki wa bongo fleva mbali kikubwa dua zenu.”

Comments

comments

You may also like ...