Header

Hat-trick ya Messi yaipeleka moja kwa moja Argentina Kombe la Dunia

CHICAGO, IL - JUNE 10: Lionel Messi #10 of Argentina celebrates his second goal against Panama during a match in the 2016 Copa America Centenario at Soldier Field on June 10, 2016 in Chicago, Illinois. Argentina defeated Panama 5-0. (Photo by Jonathan Daniel/Getty Images)

Hat-trick ya Mchezaji Bora wa Dunia mara tano Lionel Messi dhidi ya Ecuador imeipelekea timu yake ya Taifa ya Argentina katika kombe la Dunia 2018 litakalofanyika nchini Urusi.

Argentina ambayo ilikua inahitaji alama tatu katika Mchezo huo ili ijiweke katika Mazingira mazuri ya kushiriki Fainali hizo imeshinda Mchezo huo kwa jumla ya magoli 3-1 huku magoli yote yakifungwa na Lionel Messi dakika ya 12, 20 na 62 huku goli la  Ecuador likipatikana dakika ya kwanza tu ya Mchezo kupitia kwa Ibarra.

Matokeo yaliyowapa nguvu Argentina ni yale ya Brazil dhidi ya Chile ambayo Brazil imeshinda kwa magoli 3-0 ambayo yameifanya Chile ibaki na alama zake 26 huku Argentina ambayo ilikua na alama 25 ikipanda mpaka nafasi ya tatu ikiwa na alama 28 ikiungana na Brazil, Uruguay pamoja Colombia kufuzu moja kwa moja kwenye kundi hilo huku Peru ikiingia kwenye Mchezo wa mtoano dhidi ya New Zealand.

Michezo mingine iliyopigwa ya kundi hilo ni Uruguay dhidi ya Bolvia ambao Uruguay imeibuka na ushindi wa magoli 4-2 huku Peru ikitoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Colombia.

Comments

comments

You may also like ...