Header

Aslay azidi kutamba akisindikizwa na Pusha ndani ya mwezi mmoja

Kutoka Tanzania, Staa wa muziki na mkali wa ngoma kama vile Danga, Mhudumu, Likizo, Baby, Angekuona, Marioo, Pusha na nyingine kibao zilizoachiwa ndani ya muda mfupi’ Aslay ameingiza ngoma mbili katika orodha ya video za nyimbo zake zinazofanya vizuri zaidi katika mtandao wa YouTube.

Akiwa ni mwenye wimbo mkubwa  wa ‘Natamba’ uliopewa nguvu ya kuwafikia mashabiki wengi huku ukiendelea kufanya vizuri katika vituo tofauti ndani na nje ya Tanzania, imeonekana kuwa ndani ya mwezi mmoja Aslay kupitia ngoma ya ‘Pusha’ na ‘Natamba’ ambazo ndo ngoma mbili mpya zilizotoka sambamba na video zimeweza kupata watazamaji zaidi ya milioni moja ndani ya mwezi mmoja, Natamba ikiwa ni video yenye muda wa wiki moja tu tangu itoke rasmi.

Natamba ikiwa ni ngoma inayoendelea kufanya vizuri mashabiki wa muziki wa Aslay ni matumaini yao kuwa sio jambo la kustaajabisha kama watakutana na wimbo mwingine utakaotoka kimya kimya kwakuwa nje ya maoni ya kuwa Aslay anazidisha kasi ya kuachia nyimbo lakini bado inaonekana kazi zake zipokelewa uzuri na kuzifanya ziendelee kufanya vizuri zaidi.

Hata hvyo nje ya kundi la Yamoto Bendi mbali na Beka Flavour, Enock Bella na Marombosso, Aslay ni msanii mwenye nyimbo nyingi zaidi na msanii pekee aliyeonekana kuzungumziwa kwa kiasi kubwa kutokana na aina ya kipekee ya uachiaji wa ngoma bila kuwandaa mashabiki kwa namna yoyote ndani ya muda mfupi.

Comments

comments

You may also like ...