Header

Diamond akutana na mmiliki wa ‘Luc Belaire’ Brett Berish

Hatimaye Diamond amekutana na CEO wa Sovereign Brands, a Brett Berish ambaye kampuni ndiye inamiliki kilevi cha Luc Belaire kilichomfanya staa huyo kuwa mmoja wa mabalozi wake.

Diamond na Berish wamekutana nchini Marekani ukiwa ni utaratibu wa don huyo kukutana na mabalozi wa kilevi cha Belaire na kuongea masuala mbalimbali huku wakirekodiwa. Ameshafanya hivyo na Dj Khaled pia.

Chibu amepost picha akiwa na Berish na kuandika: RARE MOMENT! #BRETT
@officialbelaire #BBB #SelfMade #GoldSquad #LuxeBoys.”

Naye meneja wake, Babutale amepost picha hiyo juu na kuandika: Na mmiliki au mkurugenzi wa #Belaire nimemùonjesha diamond karanga na kanogewa na kunisisitiza mbona nimemletea chache 😂😂😂😂 kweli nogewa jirambe.”

Mwaka 2014 Brett aliuza kilevi chake cha Armand de Brignac — au “Ace of Spades” kwa Jay-Z.

Comments

comments

You may also like ...