Header

Davido aweka ushahidi mezani juu ya tuhuma zake za mauaji ya rafiki yake

Davido na Tagbo

Kutoka Nigeria, Staa wa ngoma ya ‘If’ Davido baada ya kuandamwa na tuhuma za kuhusika kwenye tukio la kufariki kwa mshikaji wake wa karibu Tagbo Umeike ‘Tagbo’ ambaye ni mtoto wa mfanyabishara maarufu nchini Nigeria, ameweka ushahidi wazi kuwa hakuhusika kutokana na maswali mengi kuibuka kuwa usiku wa kabla ya kifo cha Tagbo walikuwa pamoja katika eneo moja la kustareheka.

Video za kamera tegeshi zaClosed Circuit Television(CCTV) zilizopostiwa na Davido kupitia ukurasa wake wa Instagram, zilionesha hali halisi ya tukio na ilionekana kuwepo kwa ugomvi wakati wa kuondoka katika eneo ambalo Davido na washikaji zake walikuwa wakistarehekea na mfulilizo wa video hizo unamuonesha Tagbo akifanya mambo katika hali ya msukumo wa ulevi huku Davido akijaribu kumsaidia. Tagbo alionekana akikataa usaidizi wake Davido na baadhi ya watu wengine hali ambayo muda mfupi baadae baada ya jitihada Davido ilimuacha Tagbo na kuendesha gari akuondoka katika eneo la tukio.

Huu ndo mfulizo wa video alizopost Davido kupitia ukurasa wa Instagram juu ya kukanusha kuhusika katika kifo cha Tagbo.

Tuhuma za Davido kuonekana kuhusishwa na tukio hilo kabla ya ushihi huu wa video ziliibuliwa zaidi na Muigizaji staa wa kike kutoka Nollywood, Caroline Dunjuamo kupitia kupost aliyoweka katika ukurasa wa Instagram kisha kuiondoa ndani ya muda mfupi akidai kuwa mtu wa kwanza anayehitajika kutoa jibu la kipi kimemkuta Tagbo ni Davido kwakuwa walikuwa pamoja usiku kabla ya tukio ambapo vyombo vya usalamu nchini Nigeria katika upelelezi wa kujua undani wa tukio hilo vilitoa wito wa kuwataka Davido na muigizaji Caroline Dunjuamo kufika kituo cha polisi kwa mahojiano ya muda kisha wakaruhusiwa.

Tamko la kutoka kwa chombo cha usalama, Kamishna wa pilisi Jimbo la Lagos Mr. Imohimi Edgal

Kamishna wa Polisi wa Jimbo la Lagos, Imohimi Edgal

Kilichobaki kama swali kuu ni kuwa nimesemekana gari iliyohisiwa kumtelekeza Tagbo eneo la Hospitali kuu mjini Lagos siku ya kuamia tarehe 3 mwezi Oktoba na tukio hilo bado linapamba moto kwakuwa Davido anatajwa kuwa mtu muhimu katika kuisaidia polisi juu ya uchunguzi wa kifo cha Tagbo.

Hata hivyo mbali na tukio hilo la kufariki kwa Tagbo, bado Davido ni mwenye huzuni ya kumpoteza rafiki yake mwingine kipenzi ambaye pia alikuwa ni Dj wake, Olugbenga Abiodun ‘DJ Olu’ ambaye alikutwa kafariki ndani ya gari lake na Davido aliudhuria mazishi ya Dj huyo.

Olugbenga Abiodun (DJ Olu)

Comments

comments

You may also like ...