Header

Hamisa Mobetto na Vera Sidika warushiana matusi Snapchat

Hamisa Mobetto na Vera Sidika wameingia vitani. Wawili hao wamebadilisha matusi usiku wa kumkia leo kwenye Snapchat. Sababu ya kukosana ni Hamisa kumrekodi Vera video walipokutana barabarani jijini Nairobi alikokuwa ameenda na kuipost Snapachat.

Vera anamshutumu Hamisa kupost video hiyo kutafuta chokochoko. Ni kwasababu Vera ni rafiki yake na Zari na hivyo ameamini isingejenga picha nzuri. Wamerushiana maneno makali kwenye mtandaoni ikiwemo kuanika baadhi ya vitu vizito vinavyowahusu.

Vera amemshutumu Hamisa kufanya umalaya na kutumia watoto kama kitega uchumi kwa kuchuma fedha kwa baba zao.

Hata hivyo tayari Mange Kimambi ameununua ugomvi huo.

Comments

comments

You may also like ...