Header

Chris Brown afichua kuwa na nyimbo 800 ambazo bado hazijasikika

Staa wa muziki wa RnB kutoka Marekani Christopher Maurice Brown ‘Chris Brown’ ametoa idadi ya kustua juu ya akiba ya kazi alizo nazo mkononi ambazo haizasikika kabisa katika subira yenye hamu kubwa ya mashabiki kuigoja album yake ya nane aliyoipatia jina kulingana na panda shuka alizopitia ‘HEARTBREAK ON A FULL MOON’

Akizungumza na HOT 97 ya Mjini New York, Marekani, Chris amethibitisha tena kuwa album hiyo itatoka Oktoba 31, Siku inayofahamika kwa wengi kama siku ya Watakatifu Wote kwa jina la Halloween hata kugusia mfumo wake wa uandaaji wa nyimbo na kutoa maelezo ya akiba ya nyimbo zake kwa muda huo wa mahojiano alisema kuwa ana nyimbo 800 ambazo bado haizasikika popote.

“Kwa sasa, nimeboresha zaidi kwa sababu nimejenga studio nyumbani kwangu, kwa hiyo sijawahi kuondoka…kwenye simu yangu peke yake sasa hivi, nina kama nyimbo 800 ambazo hazijasikika kwa mtu yeyote. Sio kwamba natamaba au kujigamba lakini utaratibu wa kazi yangu unairuhusu kuwa mbunifu”aliendelea,” Ninapenda muziki na ndani ya huu muziki nina uwezo wa kutengeneza vitu kwa kiwango kikubwa, kwangu hilo mimi naliona ni baraka.” alimalizia.

Hata hivyo katika kuwaandaa mashabiki kuipokea na kufurahia kikubwa ambacho amekiandaa, Chris Brown tayari ameshaachia nyimbo tatu kutoka katika ujio wa idadi ya ngoma 45 zilizopo kwenye muunganiko wa album mbili(Double Album) zitakazo simama kwa jina moja la hilo la ‘Heartbreak on a Full Moon’.

Comments

comments

You may also like ...