Header

Otile Brown azidiwa na hisia za mapenzi ya kazi yake mpya

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya, Jack Juma Bunda a.k.a Otile Brown amegala gala kitandani kwa kile kinachoonesha kuwa amepagawa na alichokifanya katika wimbo wake mpya ‘Mapenzi Hisia’ uliokamlishwashwa na mtayarishaji Magix Enga.

Wimbo huu unaozungumzia hisia za mapenzi, umekuwa ni kazi iliofuata baada ya ile ‘Kistaarabu’ na ‘Acha Waseme’ wimbo wa mwisho uliotoka katika utofauti wa mtayarishaji ‘Ihaji’ katika hii mpya huku ikimtumia muongozaji wa video yule yule X Antonio wa International Textures ambaye ametumika katika ujio huu mwingine mpya.

Kama wazo linavyozungumza katika wimbo huu wa ‘Mapenzi hiasi’ Otile amelivaa koti la maudhui ya wimbo huo huku akihakikisha kila alichokiandika katika ushairi anakitendea haki kwa vitendo hata akionekana kulisakata ruhumba na asiache kufuata miondoko na midundo ya wimbo huu zaidi akijipagawisha zaidi katika chumba pale anapocheza na mrembo aliyevalia kimahaba mahaba mithiri ya utayari wa kubarizi ufukweni.

Itazame video ya wimbo huu ‘Mapenzi Hisia’

Comments

comments

You may also like ...