Header

Pesa ya kumkutanisha Nay wa Mitego na Youngkiller yaanza kunukia, Vipi kuhusu ‘True Boya’ jukwaani?

True Boya ni Diss track iliyoachiwa kutoka kwa Youngkiller kwenda kwa Nay wa Mitego na wengi wanaweza kusimama na kuchagua upande wa kumtetea wanayemkubali kimuziki kati ya Nay wa Mitego na Youngkiller kwa maana ya kuwa wawili hawa ni wahasimu wakubwa na wenye bifu kubwa katika muziki wa hip hop Tanznaia.

Tarehe 13 ya mwezi Oktoba 2017, Staa wa muziki wa michano Nay wa Mitego alikaa mbele ya vyombo vya habari akiwa na orodha ya wasanii kama vile QBoy Msafi, B Gway, Chemical na Pam D kisha  kuwa watamsindikiza katika ziara ya tamasha lake lililopewa jina la ‘Nguvu Ya Kitaa’ litakayofanyika viwanja vya Tanganyika Packers.

Hata hivyo hali hii yenye chembe za kibiashara inafunga milango ya bifu na utofauti uliokuwepo kwa muda ili biashara ifanyike na bila shaka mashabiki ni kiu yao kubwa kulingoja tamasha hili huku isifahamike wazi kama kipande cha uchanaji cha ‘True Boya’ ambayo ni michano iliyojaa utata wa kumchana wazi wazi Nay wa Mitego kuchanwa katika kujwaa hasa pale amshabiki wakihitaji burudani hiyo???!!!.

#NguvuYaKitaa #kidogochetukikubwachao #TanganyikaPacker's 04November

A post shared by NayTrueboy (@naytrueboy) on

Katika tamasha hili ambalo ufunguzi ni tarehe 4 Novemba wapo wengine wakali kibao ambao ni pamoja na Juma Nature, Msaga Sumu, Barnaba Classic, Gigy Money, Dully Sykes, Chid Benz, Young Killer Msodoki, Mkali Wenu na wengine ambao kulingana na makubalianao watatangazwa.

Nini Maoni yako juu ya hili kwakuwa jibu sahihi la swali linabaki katika mikono ya chumba cha habari ili kumtafuta Youngkiller aweke wazi kama ‘True boya itapata nafasi katika jukwaa la ‘Nguvu Ya Kitaa’.

 

# Tarehe #04_November_2017 Katika Viwanja Vya Tanganyika Packers "Kiingilio Elfu 3000 Tu.! Tell youR friEnd.

A post shared by M S O D O K I 🇹🇿 (@youngkillermsodokii) on

Comments

comments

You may also like ...