Header

Shabiki kufikishwa mahakamani kwa kumuingilia Justin Bieber

Ustaa ni kitu kingine kinachoweza kumsukuma shabiki kufanya kikubwa kisichotarajiwa muda wowote akipata nafasi ya kuonesha hisia zake, na huko Beverly Hills mwanamke mmoja amekamtwa akiwa katika jithada ya kuingia katika eneo la makazi ya  Staa wa muziki Justin Bieber kwa kuruka ukuta.

Siku ya Jumatatu mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 alikamatwa na polisi mara tu baada ya kutolewa kwa taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa walinzi wanahusika na usalama wa mazingira katika nyumba ya Justin Bieber.

Hata hivyo Idara ya mahakama ya mjini Beverly Hills tayari imepokea mashtaka yatakayo mkabili mwanamke huyo na kwa mujibu ya walinzi ni kuwa ni mara ya tatu sasa kwake kufanya kosa hilo la kuingia katika maeneo ya nyumba hiyo bila kuruhusiwa.

Comments

comments

You may also like ...