Header

Staa huyu wa Hollywood atumia mtindo wa Idris Sultan kumtakia happy birthday mume wake

Wakati Idris Sultan akijiandaa kuingia Hollywood hivi karibuni kwa kushiriki kwenye filamu mbili kubwa, mtindo wake wa kuwatakia birthday njema mastaa wenzake, umetumiwa na muigizaji wa Marekani, Blake Lively.

Blake ametumia Twitter kumpongeza mume wake Ryan Reynolds siku ya Jumatatu kwa kuandika, “Happy Birthday, baby,” na kuweka picha ya mwaka 2016 kwenye Critics’Choice Awards.

Hata hivyo badala ya kutumia picha nzuri ya mumewe, Lively ameweka picha ya Ryan Gosling — na huku mumewe akionekana kwa mbali upande wa kulia.

Hata hivyo, Lively ameamua kufanya hivyo kulipiza kisasi kiutani kile alichokifanya mumewe mwezi August alipomtakia happy birthday kwa kuicrop picha yake.

Huo ni mtindo ambao Idris amekuwa akiutumia siku zote, kuwapongeza mastaa kwa kutumia picha tofauti. Mfano akitaka kumpongeza Tunda, haweki picha yake bali anaweza kuweka picha ya embe au chungwa.

Lively na Reynolds walifunga ndoa September 2012 na wana wa watoto wawili wa kike, James na Ines.

Send a Letter to the Editor

Comments

comments

You may also like ...