Header

Miss Tanzania amjibu Liliane Masuka, chanzo na uwezo wa kuvaa na kupendeza

Mtagazaji wa kipindi cha mitindo Liliane Masuka amerudishiwa neno kutoka kwa Miss Tanzania 2016 Diana Edward ‘Diana Flave’ baada ya kusema kuwa amehusika kuwabadilisha Gigy Money na Diana Flave.

Akizungumza na Dizzim Online kupitia kipindi cha Home Of Stylish kinachoongozwa na Sasha Nkya, Liliane Masuka alijipongeza kuwa ameshusika pakubwa katika mafanikio ya kuwabadilisha Gigy Money na Diane Flave kimavazi kufikia hatua ya wawili hao kupendeza kila leo wanapoonekana katika matamasha tofauti.

Kilichofuata kupitia uwanja wa maoni wa akaunti rasmi ya Dizzim Online, Diana Flave alirekebisha kauli ya Liliane Masuka kwa kusema kuwa kitu kilichombadilisha ni pesa na sio jitihada za Liliane Masuka kama inavyodaiwa.

Comments

comments

You may also like ...