Header

Daxo Chali: Nimewatena Haitham na Nini sababu hawajatulia

Producer wa MJ Records, Daxo Chali amesema sababu ya kuwatema Haitham na Nini, ni wasichana hao kuwa na mienendo isiyofaa hasa katika suala zima la mapenzi. Amesema hakuwa na tatizo na wasichana hao kuwa na wapenzi, ila kilichomkata ni wao kuwa na wanaume kibao.

“Unajua kuna mahusiano halafu kuna kuwa na mtu fulani, kuwa na mtu fulani, kuna na mtu fulani… yaani sitaki niende deep sana,” Daxo aliiambia Clouds E.

Shadee alimuuliza Daxo,”Kwa kifupi walikuwa na mapenzi mengi sana yaani na watu, akiacha huyu anaenda kwa huyu hivyo eeh?” Daxo akajibu, “Issue kama hizo.”

Nini amehusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nay wa Mitego.

Comments

comments

You may also like ...