Header

Prezzo: Sina uhusiano na Amber Lulu ila ana roho nzuri sana

Rapper wa Kenya, Prezzo amekanusha tetesi za kuwa na uhusiano na video vixen aliyegeuka kuwa muimbaji, Amber Lulu. Ameiambia Dizzim Online kuwa, Lulu ni rafiki yake tu na kwamba ni mwanamke mwenye roho nzuri na huruma.

Amber Lulu ni rafiki yangu, watu wengi hawamjui, Amber Lulu ana roho nzuri sana, ana roho ya huruma na ni mtu anayewajali watu wengine,” Prezzo ameiambia Dizzim Online. “Ni mrembo kwa nje na kwa ndani,” ameongeza.

Rapper huyo amesema kuwa uhusiano wake na Amber ni kuwasaidiana na kushauriana. Kwa upande mwingine, Prezzo amekiri kuwa Amber Lulu na ameshatambulishwa kwa mama yake Prezzo na kwamba ni shabiki wake mkubwa.

Wakati huo huo, Prezzo amesema ameshafanya ngoma na Dogo Janja, Mr Blue na AY na FA.

Comments

comments

You may also like ...