Header

UMG wamtuza Diamond kwa Marry You kuuza platinum 6 na kuweka rekodi Afrika

Diamond amelibariki rasmi jina lake ‘Platnumz’ baada ya single yake Marry You aliyomshirikisha Ne-Yo kununuliwa kwa kiwango cha platinums 6. Hiyo ni rekodi ya kwanza ya msanii wa Afrika aliyesainishwa na label ya Universal Music Group.

Kutokana na hatua hiyo, leo label hiyo katika makao yake makuu ya Afrika jijini Johannesburg, Afrika Kusini, imemkabidhi staa huyo plaque kama pongezi kwa mafanikio hayo makubwa. Diamond ameandika kwenye Instagram:

Leo nimekuwa msanii wa kwanza wa kiafrika alosainiwa Universal Music Group kufikisha Mauzo ya nyimbo yake Platinum Mara sita Mfululizo kupitia nyimbo ya #MarryYou nilomshirikisha @Neyo…. kwa niaba ya Team yangu na @neyo tungependa kuwashukuru Mashabiki na Media zote Ulimwenguni

Diamond aliongoza na meneja wake Sallam, mchumba wake Zari The Bosslady na Ray Vanny kwenye kuchukua tuzo hiyo.

Zari ameandika, “Congrats babe @diamondplatnumz for becoming the first African Artist signed under Universal to hit Six times platinum sales on your #MarryYou ft @Neyo Record! Am super Proud!

Comments

comments

You may also like ...