Header

Gaga Blue awachanganya Young Dee na Amber Lulu

Staa wa kizazi cha muziki kutoka nchini Burundi anayefanya kazi chini ya usimamizi wa lebo ya muziki ya ‘U&I’, Gaga Blue amefanikisha kuwatumia mastaa wawili wa Tanzania waliopata kuzungumziwa zaidi takrinani kwa kipindi chote ambacho walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi ambao si wengine bali ni Amber Lulu na paka Rapa Young Dee.

Paka Rapa ‘Young Dee’

Kupitia kazi mbili ziliobeba maadha ya kitanzania(Bongo Touches) chini ya utayarishaji wa mkali kutoka Tanzania ‘Mr. T Touchez wa Touch Sound akishirikiana naDavy Ma-Chords ilifanyika kazi ya kwanza ambayo ilimshrikisha Young Dee kwa jina ‘Ivo Ivo’ wimbo ambao katika ushairi anasikika Young Dee akitumia lugha ya kibantu(Kirundi). Kazi nyingine ya pili ambayo imemshirikisha Amber Lulu ni hii mpya iliyopewa jina la ‘Nakupenda’ ambayo Amber ametumika kama pambo la video(Video Vixen) akishirikiana na warembo wenginen ambao sio sura ngeni kwa wafuatiliaji kwa video za wasanii wa nchini Tanznaia chini ya uongozaji wa Director Msafiri/Traveller wa Kwetu Studio.

Akiwa katika mahojiano na Dizzim Online, Gaga Blue alizingumzia kwa kina safari ya muziki wake. kutoka Burundi mpaka Tanznaia na  jinsi ilivyowezekana kufanikisha nyimbo hizo mbili ndani ya muda mfupi wa kipindi ambacho ametumia muda wake kufanya muziki wake nchini Tanzania.

Itazame ‘Ivo Ivo iliyomshirikish Young Dee.

Comments

comments

You may also like ...