Header

Aslay aanza kutamba kwa Zawadi hii kutoka kwa Menejimenti yake

Staa wa muziki wa Bongo Fleva na mkali wa ngoma ‘Natamba’ ameanza kukwea mlima wa matunda ya anachokifanya kwa sasa kwa kuipokea zawadi ya Gari alilopewa na uongozi wa Menejimenti yake anayofanya nayo kazi kwa kipindi chote alichoanza kufanya kazi za muziki wake nje ya Yamoto Band.

Kupitia ukurasa wake wa Instgram Aslay ameweka picha ya Gari ‘BMW’ huku akiwa amejiachia na mwane ‘Moza’ juu ya gari hilo nakuandika maneno ya kuwashuruku wahusika katika uongozi wa menejimenti yake ambao ni ‘Chambuso’ na ‘Mx Carter’.

Hata hivyo katika mfumo ule ule wa kuachia nyimbo mtawalia/mfulizo, Aslay amendeleza hali hiyo  kwa kuachia kimya kimya wimbo wake mwingine mpya alioshirikiana na muimbaji wa kike Nandy unaokwenda kwa jina la ‘Mahabuba’ chini ya utayarishaji wa producer Shirko katika studio za Vibe Records.

Comments

comments

You may also like ...