Header

Iyanya wa miaka 31, aingia katika orodha ya wasio na Mpenzi

Kutoka nchini Nigeria, Staa wa ngoma ya ‘Kukere’ Iyanya Onoyom Mbuk a.k.a Iyanya ametimiza miaka 31 na anasherehekea siku yake muhimu kwa kutakiwa heri na ndugu, jamaa na marafiki pekee mbali na kuwa kati ya mastaa wa kiume wenye mvuto wa kimapenzi kwa akina dada.

Cha tofauti katika siku hii ya leo ambayo ni kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa Staa Iyanya, ni kuwa ametimiza umri wa miaka 31 akiwa katika headlines za kuwa hana mpenzi na hayuko katika mahusiano ya kimapenzi na mrembo yeyote kwa mujibu wa alichokisema katika mahijiano yake ya hivi karibuni na Saturday Beats ya Nigeria ambapo alitoa sababu za kwanini anaamua kuishi hivyo mbali na kuwa anawindwa na wanaolitamani penzi lake na mvuto wake.

Miongoni mwa sababu alizotoa Iyanya juu ya kuendelea kuwa single/kipekee pekee yake kimahusiano ni kazi za hapa na pale zisizompatia wasaa wa kuyafikiria kwa kina maisha ya mahusiano ingawa alibainisha kuwa muda wowote anaweza kupata mwanamke wa kuwa naye hata kama hasingekuwa msanii na alisawazisha kuwa hayuko katika mahusiano hata kuhaidi kuwa hilo la mahusiano na mwanamke litafika tu na hakuna nayejua ni lini na kwa nani.

Hata hivyo kwa Iyanya ambayo katika mahusiano yake yaliyopita kwa Yvonne Nelson na kwa Freda Francis ambayo hayakuisha vizuri, katika siku hii ya kuzaliwa kwake hatapata maneno ya heri ya wazazi wake na kaka yake mkubwa ambao walifariki katika kipindi cha mwaka 2008 na mwaka 2010. Iyanaya katika kuwakumbuka na kuwapa heshima katika maisha yake, mwaka 2014 alichora tatoo katika mwili wake eneo la kifua na kuandika majina yao kumbukumbu inayobaki katikamakili yake na mwili wake.

 

 

Comments

comments

You may also like ...