Header

Jaguar ampa mkono wa Pongezi ya Urais ‘Uhuru Kenyatta’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mbunge wa jimbo la Starehe lililopo Nairobi nchini Kenya, Charles Njagua Kanyi a.k.a Jaguar amempongeza Uhuru Kenyatta kwa hatua yake ya ushindi wa marudio ya uchaguzi wa mwaka huu na kutangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa idadi ya kura 7,483,895 ambayo ni sawa na 98% ya matokeo ya Uchaguzi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jaguar amempongeza Uhuru Kenyatta katika matokeo ambayo kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo katika nafasi ya pili alipata jumla ya kura 73,228 sawa na asilimia 0.96 akifuatia Mohamed Abduba Dida aliyepata ushindi wa jumla ya kura 14,107 sawa na asilimia 0.19.

 

Hata hivyo Jaguar ambaye nje ya kuwa kijana maarufu nchini Kenya kwa kupeperusha bendera ya sanaa ya muziki, bado ni mwanasiasa ambaye katika hili la ushindi wa Uhuru Kenyatta amewakumbusha Wakenya kuzingatia Amani na Upendo kwa Taifa la Kenya katika msimu huu mpya wa kumkabidhi jukumu Kenyetta kuongoza miaka mingine mitano.

Comments

comments

You may also like ...