Header

Mkongwe Dj Juice Afariki Dunia

(Kulia) Dj Mackay akiwa na Dj Juice enzi za uhai wake

Dj wa muda marefu na mkongwe katika tasnia ya muziki na Burudani Tanzania, Hussein Juma a.k.a Dj Juice amefariki Dunia usiku wa kuamkia tarehe 31 katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa rafiki yake wa karibu ambaye wameshiriki mara kadhaa katika kazi za pamoja, Dj Mackay alitoa taarifa za msiba huo kwa kutoa salamu za pole kwa familia ya ndugu jamaa na marafiki na kuongeza kuwa shughuli za mziko ya Dj Juice zitafanyika jioni ya siku ya jumanne(leo) mida ya saa 10 jioni katika Makaburi ya Ndungumbi, Magomeni Makuti jijini Dar es Salaam.

Taarifa za watu wa karibu wa Dj Juice hazibainishi hasa nini kilimsumbua Dj Juice mp zaidi ni kuwa aliugua na kuanza kupata matibabu ndani ya muda wa wiki moja kabla ya kukutwa umauti usiku wa kuamkia jumanne wa tarehe 31 ya mwezi huu wa Oktoba.

Comments

comments

You may also like ...