Header

Wizkid kubariki kipaji cha Producer Chipukizi katika hali ya mzaha

Mwimbaji nyota kutoka nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun a.k.a Wizkid ametoa nafasi ya kipekee na ya matumaini kwa mtayarishaji wa midundo na muziki katika hali isiyotegemewa.

Mtayarishaji huyo anayechipukia katika utayarishaji wa muziki anayejitambulisha kwa jina Jaylon, kupitia mtandao wa Twitter aliweka video iliyosikika ukichezwa mdundo alioutengeneza, mdundo ambao muda mfupi baadae mshikaji mmoja kwa jina @heen_benny alitoa maoni ya kuwa mdundo ule vipi kama atautumia Wizkid.

Katika maoni ya kuwa mdundo ule itakuwaje kama atautumia Wizkid, Basi Wizkid alijibu maoni kwa kutaka atumiwe mdundo huo kitu ambacho kimewafanya wengi walioona mfululizo wa jambo hilo kuamini kuwa Wizkid atafanya kazi juu ya mudundo huo.

Hata hivyo hii ni bahati ya kipekee na kubwa kwa Jaylon kwakuwa upo uwezekano mkubwa kwake kuwa atazungumziwa zaidi pindi kazi mpya ya Wizkid itakapotoka yenye kutumika kwa mdundo wake huo.

Comments

comments

You may also like ...