Header

Aime M. kuukwea mlima wa Umaarufu kistaa zaidi

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Burundi, Aime M. ameingia katika orodha ya wasanii wanoishi na kufanya zao nje ya nchi yao huku wasiache kuzingatia uzalendo wa nchi yao na njia zote zile za wasanii wakubwa Duniani wenye kufuata mfumo wa teknologia katika sura ya biashara ya muziki.

Aime anayefanya vizuri kupitia kazi yake ‘Mapenzi’ ailiyoingia sokoni mwanzoni mwa mwaka huu wa 2017, anaenedelea kufanya kazi akiwa katika makazi yake ya kudumu nchini Marekani ambapo amehakikisha kila jukwaa la kuuza muziki hasa mitandaoni ameweka nyimbo zake akiamini kuwa mbali na kasi yake ya kuongeza mashabiki kila leo, lakini bado anajipa thamani ya kuuza muziki wake kama ilivyo kwa wasanii wengine wenye majina makubwa.

Hata hivyo Aime M, katika kulikuza jina lake na kuupa thamani ya juu muziki wake, ameshabahatika kukutana uso kwa uso na Mastaa wenye majina makubwa katoka katika mataifa yanayozungumza lugha nayoielewa hata kuitumia katika muziki wake yaani Kiswahili na Kifaransa ambao ni pamoja na Diamond Platnumz na Rayvanny kutoka Tanzania na Fally Ipupa kutoka Kongo.

Aime M akiwa na Diamond Platnumz na Rayvanny

 

Aime M akiwa na mkongwe Fally Ipupa

Vile jitihada za kuyafahamu mengi juu ya aina hii ya muziki anaofanya na mfumo anaotumia nchini Marekani zinaendelea na chumba cha habari cha DIzzim Online kitakupakulia mengi mazuri.

Comments

comments

You may also like ...