Header

Godzillah athibitisha ujio mwingine na Young Dee

Rapa na mkali wa mitindo huru(Freestyle) kutoka Sala Sala jijini Dar es Salaam ,Tanzania, Golden Jacob a.k.a Godzillah, amewaweka tayari mashabiki juu ya ujio wa kazi yake aliyomshirikisha Paka Rapa Young Dee kuwa iko njiani kutoka hivi karibuni.

YOUNG DEE. Picha kwa Hisani ya Instagram/ Young Dee

Akiwa ni mwenye kuonjesha tu kidogo juu ya taarifa hiyo kuwa ataachia kolabo hiyo, Godzillah hakuwa tayari kuitaja siku rasmi ya kuachia kazi hiyo bali kikubwa ni kuwaweka mashabiki katika utayari wa kopokea kazi yake mpya.

Hata hivyo katika kolabo hiyo, haitakuwa mara ya kwanza kwa Godzillah na Young Dee kukutana katika wimbo kwakuwa walishaikutanisha michano yako katika kazi waliyoshirikishwa na rapa Giddy katika ngoma ‘One Minutes’.

Comments

comments

You may also like ...