Header

Michael Jackson ashika nafasi ya kwanza kifedha

Mfalme wa muziki wa Pop Duniani aliyefariki Dunia miaka minane iliyopita, Michael Jackson ameingia tena katika orodha ya wasanii wanaoingiza mkwanja mrefu katika orodha ya wasanii wa Tano wakubwa Duniani.

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na jarida la Forbes ya Watu maarufu waliofariki dunia, Michael Jackson ameshika nafasi ya kwanza kwa kutengeneza kiasi cha dola za kimarekani Milioni 75 kwa mwaka 2017 kupitia kazi zake za sanaa alizoachia enzi za uhai wake na nyingine zilizotoka kipindi ambacho alikuwa ameshafariki Dunia.

Hata hivyp huu ni mwaka wa tano mfululizo kwa MJ kukaa kwenye kilele, huku Forbes wakisema fedha hizo zinaingia kupitia mauzo ya album zake za karibuni ambazo ni pamoja na Scream yanaoendelea, mgao wa mapato kutoka kampuni ya muziki ya ‘EMI Music Publishing Ltd’ ya Uingereza na mapato Kwenye show ya Las Vegas Cirque du soleil.

Hii ndio orodha ya Mastaa wanaokamilisha Top 5.

1. Michael Jackson ($75 million)
2. Arnold Palmer ($40 million)
3. Charles Schulz ($38 million)
4. Elvis Presley ($35 million)
5. Bob Marley ($23 million)

Comments

comments

You may also like ...