Header

Aslay awadanganya mashabiki kumtetea Enock Bella

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mkali wa ngoma ‘Natamba’ Aslay ameonekana kuwa msanii aliyediriki kuwadanganya mashabiki kwa mgongo wa ndoa kama njia pekee ya kuutetea ujio wa kazi mpya ya msanii mwenzake Enock Bella.

Itakumbukwa kuwa kati ya wasanii waliounda kundi la Yamoto Bendi, ukiachana na Aslay, Beka Flavour na Marombosso pia Enock Bella alikamilisha idadi ya wanakikundi hicho kipindi ambacho walifanya kazi za pamoja. Baada ya maneno maneno yenye tetesi na uvumi wa hapa na pale juu ya kuvunjika kwa kundi hilo, basi kila mmoja alionekana kujitawala katika sura ya kuachia kazi ya pekee yake ambapo utaratibu huo uliongozwa na Aslay.

Wengi walionekana kumpokea vyema Aslay ambapo Beka Flavour naye alipokelewa vyema kupitia kazi yake ya ‘Libebe’ na ‘Sikinai’ huku wengi wakiutamani ujio wa Enock Bella, ukiachana na Maromboso aliyekwisha anza kufanya kazi chini ya usimamizi wa lebo ya Muziki ya WCB Wasafi.

Oktoba 23 mwaka huu wa 2017, Aslay aliutumia ukurasa wake wa Instagram kuwadanganya mashabiki kwa bashasha za pongezi kwa hatua ya msanii mwezake Enock Bella kuchukua jiko(Yaani kupata mke/Kuoa). Katika picha Enock alionekana akiwa ni mwenye kujistili kwa suti ya gharama akiwa kamkaribiria mrembo mmoja kwa jina maarufu ‘Mami’ aliyejipamba kwa nakshi ya vazi la heshima mithiri ya Bibi Harusi.

Kilichokuja kugundulika usiku wa kuamkia tarehe 3 ya mwezi Novemba, Enock ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Sauda’ uliotayarishwa chini ya Studio za WCB Wasafi kwa mkono wa Lizer Classic huku video ikiongozwa na Director Ivan ambapo mrembo aliyetumika katika video hiyo ndo yule ambaye alitajwa kama mke wa Enock Bella katika picha aliyopost Aslay mrembo akiwa sambamba na Enock Bella.

Hongera sana Damu Yangu Kwa Kuchukua Jiko Safi Sana @enockbellaofficial Dah Safi Sana Ndugu Yangu

A post shared by Aslay (@aslayisihaka) on

Hata hivyo kingine ambacho kimetambulishwa rasmi kwa wengi ambao wanamfahamu na kumfatilia Enock Bella ni kusikika akijiita Enock Bella ‘Base’ kutokana na haina ya sauti anayoitumia katika uimbaji wake.

Itazame Video ya wimbo wa Enock Bella.

Comments

comments

You may also like ...