Header

Justin Bieber na Selena Gomez wamerudiana rasmi, fahamu nani alimuanza mwenzake

LOS ANGELES, CA - APRIL 17: Selena Gomez (L) and Justin Bieber attend a basketball game between the San Antonio Spurs and the Los Angeles Lakers at Staples Center on April 17, 2012 in Los Angeles, California. (Photo by Noel Vasquez/Getty Images)

Justin Bieber ndiye aliyemuimbisha Selena Gomez, na sio vinginevyo. Na pia haikuwa rahisi kufanya hivyo. Alijitahidi kumshawishi kwa muda kuwa kurejesha tena uhusiano wao ungekuwa kitu kizuri.
Vyanzo vilivyo karibu na wote, Justin na Selena vimeiambia TMZ kuwa upasuaji wa hatari aliofanyiwa Selena wa kuwekea figo nyingine ulimbadilisha Justin.

Chanzo kimoja kimesema Bieber hakujua jinsi ambavyo bado anampenda hadi alipobaini kuwa anaweza kufa na hiyo ilimfanya afikirie tofauti. Justin alimuimbisha Selena wakati akiwa na na uhusiano bado na The Weeknd, ingawa uhusiano wao ulikuwa ushaanza kuyumba.

Ndugu zake na Selena hata hivyo hawakubariki kurudiana kwake na Justin kwasababu wanamlaumu kwa kumpa msongo mkubwa wa mawazo Selena hadi kwenda rehab. Kuna ripoti pia kuwa uhusiano wao unaelekea zaidi kimuziki na sio mahaba, kwamba wakiwa pamoja wanakuwa na nguvu zaidi.

TMZ imethibitisha kuwa wamerudiana kabisa kwa sasa.

Comments

comments

You may also like ...