Header

Linex aandaa album, atoa idadi kamili ya nyimbo kabla hazijakamilika

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Linex Sunday Mjeda, amethibitisha kukamilisha nusu ya idada ya nyimbo ishirini zitakazo unda Album yake inayotarajiwa kutoka siku za usoni.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Muimbaji huyo anayemiliki kundi la muziki la Voice Of Africa (VOA) ameandika kuwa yuko katika hatua ya kukamilisha wimbo wa kumi na nne, wimbo ambao imeonekana kuwa umetayarishwa na Producer Mr T Touch wa Touchez Sounds.

Hata hivyo Linex kwa sasa anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake ‘Got Me’, wimbo ambao bado haijabainika kama utapatokana katika orodha ya nyimbo zitakazo patikana katika Album ijayo ya Linex.

Comments

comments

You may also like ...