Header

Nasikitika watu kudhani ndoa yangu na Irene Uwoya ni kiki – Dogo Janja

Dogo Janja amesema kitu kinachomsikitisha ni watu kuchukulia kuwa ndoa yake na Irene Uwoya ni kiki.

Amesema kitu hicho ndicho kiliwafanya wafanye ndoa na uhusiano wao siri ili kuepuka na watu kudhani wanaigiza tu. Amesema hayo leo kwenye mahojiano yake ya kwanza tangu afunge ndoa kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

“Mimi pia inakuwa inaniumiza sana na inabidi watu wajue kuwa nimeoa kweli,” alisema.

“Mimi sio mtu wa drama drama, nimeoa, nimefanya nusra ya dini. Familia yangu imetoa baraka zote kwasababu kwanza mimi nilishawahi kwenda nyumbani na Sheila [Irene] na kiukweli mama alimfurahia sana, alikuwa yuko happy naye, tulicheka sana, nikamuambia ‘mama basi mimi nampenda sana huyu mwanamke, nitamuoa ili uendelee kufurahi zaidi.”

Irene na Dogo Janja walifunga ndoa Ijumaa iliyopita. Irene Uwoya amebadilisha dini na jina lake kuwa Sheila.

Comments

comments

You may also like ...