Header

Barakah The Prince amuachia Mungu watu wanaomrudisha nyuma kimuziki

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mmiliki mwenza wa lebo ya muziki ya BANA MUSIC, Barakah The Prince ameweka mtandaoni maelekezo yenye malalamiko yaliyoibua hisia za kuwa kuna uwezekano wa kuwa kuna jambo ambalo haliko sawa katika akaunti yake ya mtandao wa YouTube.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Barakah ametuma picha ya kukamata skrini yenye maelezo na ujumbe moja ya watu waliogundua tatizo linaloendelea katika akaunti yake hiyo, matatizo yakionekana kuwa kuna hali ya mabadiliko ya mfumo wa kufikiwa kwa video tofauti na anlivyoweka yeye kwenye wimbo wake mpya wa ‘Sometimes’.

Hata hivyo Barakah katika kazi hii mpya ya ‘Sometimes’ inahesabika kuwa ni kazi yake ya kwanza kuachiwa chini ya lebo yake hiyo ya BANA MUSIC.

Comments

comments

You may also like ...