Header

Dogo Janja asonga mbele baada ya kukamilisha jukumu la Ndoa

Staa wa ngoma ya ‘Ngarenaro’ Abdulaziz Abubakari ‘Dogo Janja’ amegeukia misingi ya kazi yake kama msanii baada ya wiki ndefu iliyopita iliyobeba mjadala marefu wa ndoa yake na mrembo toka kwenye tasnia ya filamu Tanzania ‘Irene Uwoya’.

Dogo Janja ambaye kazi yake ya ‘Ngarenaro’ ilifanyika chini ya utayarishaji wa studio za ‘Suprise Music’ zenye umiliki wenza wa msanii Rayvanny, Sasa ameingia studio kwa pishi la kazi nyingine chini ya tayarishaji wa producer Daxo Chali wa MJ Records.

Back To Tha Bizz!! #StudioLife W/ @daxochali #NightSession #TeamNoSleep

A post shared by Dogo Janja (@dogojanjatz) on

Dogo Janja anayefanya kazi chini ya usimamizi wa Tip Top Connection anaendelea kuwa kati ya wasanii wenye nafasi ya kufanya vizuri kutokana uzuri na ubora wa kazi zake  na kuwa katika orodha ya wakali wenye jihitada za kuachia wimbo kila kiu ya mashabiki ikimtaka kufanya hivyo bila kupoteza muda.

Comments

comments

You may also like ...