Header

Octopizzo awaruka wazi wazi vijana wavivu mitaani

Rapa kutoka nchini Kenya, Henry Ohanga a.k.a Octopizzo amewapa changamoto kubwa ya kimaenedeleo vijana hasa wanaopata msukumo na motisha ya kutoka hatua moja hadi nyingine katika umri wa ujana.

Akizingatia mfumo wa vijana kuwa nguzo na nguvu kazi ya taifa, Octopizzo ameweka ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter akiwalenga vijana akionesha kutopendezwa na baadhi ya tabia za baadhi wanaopenda kukaa vijiweni na kupiga soga  wakingoja kusaidiwa na vijana wenzao waliojituma na kufikia hatua ya mafanikio.

Octopizzo katika twitte yake ametumia ya mtaa(Sheng) inayoeleweka zaidi nchini Kenya katika maeneo machache yanayozingatia lugha hiyo ya kimtaa zaidi.

Kwa kiswahili kiachoeleweka kwa wengi Octopizzo alisema.

“Sisalimii vijana wanaokaa vijiweni mimi sio MP, Mimi usalimia watu wako katika miangaiko ya kazi. Ukisubiria nije mtaa kukusalimia utangoja sana” Octopizzo Aliandika.

Hata hivyo ujumbe huo wa Octopizzo ni changamoto kwa vijana wote wenye nia na malengo ya kufikia ndoto zao kwakuwa Octopizzo ni Staa wa muziki wa rap aliyefanikiwa kutoka katika eneo la watu wa maisha na kipato cha chini nchini Kenya linalofahamika kwa jina ‘Kibera’.

Comments

comments

You may also like ...