Header

“Siwezi kuongelea suala la mwamuzi mi sijui chochote”-Kichuya

Kiungo wa Klabu ya soka ya Simba Shiza Ramadhani Kichuya amesema kuwa hajui kitu chochote kuhusiana na Maamuzi ya Mwamuzi wa Mchezo wao wa jana dhidi ya Mbeya City bali anachojua yeye ni kuwa Timu yake imepata pointi tatu katika Mchezo huo.

Kichuya ambaye alifunga goli dakika ya 7 ya Mchezo likiwa ndio goli lilowapa Alama tatu Wekundu wa Msimbazi katika Dimba la Sokoine amezungumza na kituo cha Azam tv kutoka jijini Mbeya baada ya Mchezo na kusema kuwa suala la Mwamuzi halimuhusu wala haliwahusu wachezaji wote wa Simba wanachojua wao wamepata alama tatu katika Mchezo huo Mgumu.

“Siwezi kuzungumzia suala la Mwamuzi kwa sababu mimi sijui chochote mi nachoangalia ni kitu gani nafanya Uwanjani na tunacheza vipi sisi kama Simba suala la Mwamuzi sisi hatujui labda wao (Mbeya City) na watu wengine”. Alisema kichuya mbele ya Camera za Azam tv.

Pia Kichuya ameelezea goli lake ambalo watu wengi wanasema kuwa alikuwa offside na kwamba Mwamuzi hakuona hilo huku yeye akidai kuwa alitumia ujanja kuiua Offside.

“Mimi nimeomba mpira  kutoka pembeni nikamzunguka beki kwa mbele unapomzunguka beki kwa mbele inakuwa sio Offside unakua umeshaiua ingekua nimemzunguka kwa nyuma ndio ingekuwa offside”

Simba imepaa mpaka kileleni mwa Ligi kuu Tanzania bara baada ya Mchezo wa jana ikifikisha jumla ya Alama 19 sawa na Klabu ya Azam ambayo imezidiwa Magoli ya kufunga na kufungwa.

 

 

Comments

comments

You may also like ...