Header

Diamond Platnumz aungana na Mastaa kibao Duniani kumtia moyo rapa Meek Mill

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ameungana na mastaa kibao Duniani katika mchakato wa kuutetea uhuru na kumtia moyo Rapa na staa wa muziki kutoka Marekani Meek Mill aliyehukumiwa kifungo cha miaka 2-4 jela hukumu iliyotoka wiki hii.

Kwa rapa Meek Mill ilifahamika kuwa atayaishi maisha ya jela kwa muda wa miaka 2-4 baada ya hukumu ya kosa na kukiuka mashariti ya kuishi chini ya uangalizi wa kisheria wa maosa yake ya kesi ya mwaka 2009 iliyomkabili kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria na ushahidi wa kukutwa na mdawa ya kulevya.

Meek Mill aliingia katika matatizo makubwa haya ya kuishi nyuma ya nondo za gereza baada ya tukio la kupigana uwanja wa ndege na makosa mengine ambayo ni sambamba na kosa na kuendesha pikipiki kwa fujo mjini New York.

Hata hivyo lebo yenye mkataba wa kikazi na rapa Meek Mill, Mayback Music Group(MMG)  kupitia ukurasa wa twiter imetoa ujumbe wa mtumaini ya kuwa Meek atarudi na litakuwa ni jambo kubwa sana akionekana tena uraiani na lebo hiyo mebaki na jukumu la kuwakilisha vilivyo.

Vile vile Dj Kaled aliguswa zaidi hasa kuguswa zaidi na maumivu ya rapa Meek Mill kuishi mbali na mwane, marafiki wa karibu na familia yake kwa ujumla.

Comments

comments

You may also like ...