Header

Je? AliKiba kuikata kiu ya mashabiki na kazi nyingine kwa hiki kinachoonekana?

Staa wa muziki wa bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ ameanza kuonesha dalili za ujio wa kazi nyingine baada ya ‘Seduce Me’ iliyoingia kwenye rekodi ya kazi zake zilizopokelewa vizuri zaidi ndani ya muda muda mfupi kwa mwaka 2017.

AliKiba sio mtu wa maneno mengi katika kuachia kazi zaidi ya vionjo vya kugusia gusia kwa maneno machache ya kinachopatikana katika kazi yake yoyote pindi anapoelekea kuiachia rasmi ambapo mapema leo aliweka picha yake akiuliza mashabiki kuwa nini ‘Kinafuata?? ‘What Next…?.

What Next …? #KingKiba

A post shared by alikiba (@officialalikiba) on

Muda mfupi baadae mara baada ya post hiyo iliyoambatana na swali, Kiba aliweka picha yake nyingine akiwa na muongozaji wa video mpya ya kolabo ya wimbo ‘Malo’ wa Tiwa Savage uliyowashirikisha StarBoy ‘Wizkid’ na SpellzDirector Meji Alabi. Swali likaibuka Je’ anachouliziwa kuwa nini kifuate kimeongozwa na Director Meji Alabi ambaye aliongoza video ya hitsong ya ‘Chekecha Cheketua’ ya AliKiba.

@mejialabi 🙌🏻🙌🏻 #KingKiba

A post shared by alikiba (@officialalikiba) on

Kwa muendelezo huu wa picha za AliKiba kupitia ukurasa wake wa Instgram imedhaniwa kuwa kuna uwezekanao wa kuwa kuna Video inakuja??

Swali hilo jibu lake analo AliKiba, Director Meji Alabi na uongozi wa RockStaa4000 hivyo mashabiki wanahitaji kuwa tayari muda wowote kwakuwa AliKiba alishawahakikishia mashabiki kuwa msimu huu hata weka ukimya wa muda mrefu sana kama alivyokuwa akifanya kipindi cha uachiaji wa kazi zake za nyuma.

Comments

comments

You may also like ...