Header

Ruby asema kuimba na CD jukwaani ni adhabu kubwa kwake

Wasanii wengi wa Bongo Flava hupenda zaidi kutumbuiza kwwa CD jukwaani, lakini si kwa Ruby. Ameiambia Dizzim Online, “Yaani mimi napenda kuimba live kwasababu nishazoea kuimba live tangu mdogo. Kwahiyo mimi kuimba kwenye CD kitu ambacho bado nafanyia mazoezi, ameongeza.

CD inaninyima uhuru unajua nikiimba live naweza kucheka, naweza kuongea na mashabiki pia na bado nikarudi pale pale so napenda kuimba live.”

Ruby amewaomba mashabiki zake waendelee kuwa na subira juu ya kazi zake mpya.

Comments

comments

You may also like ...