Header

Twitter watoa huduma mara mbili ya ile ya awali

Mtandao wa kijamii wa Twitter umeongeza ubora wa huduma ya watumiaji waliotamani kuongezewa idadi ya maneno/tarakimu na alama za kutuma ujumbe katika kurasa zao binafsi na safu za maoni.

Kupitia ukurasa rasmi wa Titter, ulitumwa ujumbe kuwa wanatanua wigo kwa kupunguza mashariti ya kizuizi cha idadi ya tarakimu 140 pekee. Twitter ilitangaza kuwa baadala ya tarakimu 140, mtumiaji anaweza kutuma ujumbe wenye tarakimu 280 yaani mara mbili ya huduma ile ya awali.

Hata hivyo miongoni mwa sababu kubwa za mabadiliko hayo ni pamoja na kuweka urahisi wa mtumiaji kujieleza kupitia Twitter kwa haraka zaidi.

Ujumbe kutoka kwetu kupitia Twitter ulithibitisha hilo baada ya kutumia maneno zaidi ya 140 katika safu ya kutuma ujumbe kuhusu mbadiliko hayo ya Twitter.

Comments

comments

You may also like ...