Header

Otile Brown asema ukweli wa kutofahamu jambo kuhusu Rihanna

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya, Jack Juma Bunda a.k.a Otile Brown ameruka mita mia juu ya yeye kufahamu chochote kuhusu kuonekana kwa makusudi na kufanana kwa mchoro wa tattoo ya mrembo ‘Tatiana’ aliyetumika katika video ya wimbo wake mpya ‘Mapenzi Hisia’.

Tattoo ya Rihanna inayofanana na Marembo Tatiana

Akipiga stori na Dizzim Online, Otile Brown amesema kuwa hakufahamu kuwa tattoo ile inayoonekana chini ya kifua cha video queen Tatiana ilishapa umaarufu kwa kuchorwa na mrembo muimbaji kutoka Marekani, Robyn Rihanna Fenty a.k.a Rihanna.

“Tatiana ni a Super Model kutoka hapa nchini Kenya na ni mwanabiashara, Nilipokuwa nafanya video ya mapenzi hisia sio kwamba nilikuwa na nia ya kupata mtu mwenye tattoo kama hiyo, maana sikujua kama amechora tattoo kama hiyo ya Rihanna.

Sasa hivi ndo nimegundua baada ya wewe kuniuliza ndo nikagundua Ahaa! kweli kumbe zinafanana. Ilitokea tu, nilimtaka yeye kwenye video na ilipofika wakati wa scene ya wimming pool na vitu kama hivyo ndo nikapata kuiona hiyo Tattoo. Nilikuwa sijui ila sasa najua” Amesema Otile Brown.

Hata hivyo video ya wimbo huo wa ‘Mapenzi Hisia’ umeongozwa na Director X Antonio na inawezekana alipenda tattoo hiyo itumike kupamba video kwakuwa aliionesha katika sura ya kuweka kuwa rahisi kubaki katika vicha vya watazamaji watako bahatika kuiona video hiyo.

Comments

comments

You may also like ...