Header

Ndugu wa Nicki Minaj jela kwa kosa ya Ubakaji

Ndugu wa kiume wa Rapa wa kike, Onika Tanya Maraj ‘Nicki Minaj’, Jelani Maraj amepatikana na hatia ya kutenda kosa la unyanyasaji wa kingono wa mtoto wa Long Island katika kesi iliyodumu kwa muda wa takaribani  wiki tatu.

Jelani Maraj, mwenye umri wa miaka 38, anakabiliwa hukumu ya kwenda jela na kuishi maisha ya gerezani baada ya kuhukumiwa kwa kosa hilo la unyanyasaji wa kijinsia wa kingono unaokiuka haki kisheria dhidi ya mtoto mwenye umri wa miaka 11 nyumbani kwake huko Baldwin.

Jelani Maraj

Uamuzi wa Jelani Maraj baada ya kupatikana na kosa hilo umetoka Alhamisi hii huko Long Island na baada ya Jelani kupatikana na makosa hayo, kisheria anakabiliwa na hukumu ya miaka 25 jela ambapo hukumu itafanyika Desemba 14.

Comments

comments

You may also like ...