Header

Leonardo DiCaprio wa Titanic agonga 43 kuelekea Ukongwe

Staa wa filamu kutoka Marekani, Leonardo DiCaprio ni miongoni mwa Mastaa wenye heshima ya kushiriki katika filamu nyingi kubwa na siku ya tarehe 11 Novemba mwaka 1974 aliufungua ukurasa wa Maisha yake kwa heshima ya uzazi wa Baba yake, George DiCaprio na mama yake Bi. Irmelin Indenbirken. Na leo Leonardo DiCaprio anatimiza umri wa miaka 43.

Leonardo DiCaprio na Kate Winslet

Umaarufu wake wa kushiriki katika filamu kubwa na maarufu Duniani, Leonardo DiCaprio kama ‘Jack Dawson’ akiwa ni mpenzi wa Kate Winslet kama ‘Rose DeWitt Bukater’ alifanikiwa kuingia kwenye vichwa vya wengi kupitia filamu ya ajali mbaya ya kuzama kwa Meli Kaskazini mwa Bahari ya Atlantic, filamu iliyoigizwa mwaka 1997.

Picha za kumbukumbu ya meli ya Titanic

Leonardo DiCaprio na Rose DeWitt Bukater

Meli hiyo iliyobeba maudhui ya kuzama katika filamu ‘Titanic’ ilizama mwaka 1912, na takribani watu wasiopungua 1500 walipoteza maisha katika harakati za kujioko na wengine kupata msaada wa kupona ajali hiyo iliyotandaza simanzi katika sura za wengi walioguswa na tukio.

Ukurasa wa Mbele wa Gazeti la ‘The Boston Daily Globe’ ulitoa taatifa ya kuzama kwa ‘Titanic’

Kampuni ya meli ya Blue Star Line tayari imetengeneza meli ya Titanic yaani Titanic II ambayo imefanana kwa asilimia kubwa na ile ya awali iliyozama baada ya kugonga kipande kikubwa cha barafu kilichosababisha kutoboka kwa chini kwa meli hiyo hata kusababisha maji mengi kuingia ndani.

 

Titanic II

Hata hivyo Leonardo DiCaprio, katika ubora wake wa kuigiza mbali na wengi kumjua kupitia Titanic lakini pia ametokea katika filamu kadhaa na kubwa kama vile The Revenant, The Wolf of Wall Street, Romeo And Julieth, Inception, The Departed, The Aviator, Shutter Island na nyingine kibao ambazo zinahesabika katika ramani ya wapenda filamu Duniani.

Comments

comments

You may also like ...