Header

Davido aendeleza utaratibu wake wa kazi na FIA(FIRE)

 

Mapema soko la muziki Afrika limepokea kazi mpya ya msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria David Adedeji Adeleke ‘Davido’ aliyetamba na ngoma kama vile ‘FALL’ na ‘IF’. Davido ameachia wimbo unaoitwa ‘Fia’ uliotoka sambamba na Video chini ya uongozaji wa Director Clarence Peters.

Fia ukiwa ni wimbo uliotayarishwa na producer Fresh, ni moja ya nyimbo zitakazopatikana katika albamu mpya ya Davido itakayofuata inayotarajiwa kutoka muda wowote baada ya ‘Son of Mercy’ iliyotoka mwishoni mwa mwaka jana(2016).

Hata hivyo Davido wengi wamebahtika kupata burudani kubwa ya muziki wake katika ziara yake ya Dunia ya ’30 Billion World Tour’ iliyomalizikatamati nchini Guinea, Septemba 16 ya mwaka huu. mwaka huu ambapo ilizunguka katika miji mbalimbali nchini Marekani, Ulaya na Afrika.

Angalia video hapa chini:

Comments

comments

You may also like ...