Header

Alikiba na Nandy waibuka kidedea tuzo za Afrima 2017

Alikiba na Nandy jana Jumapili waliibuka na ushindi kwenye tuzo za Afrima zilizofanyika jijini Lagos, Nigeria. Kiba ameshinda tuzo mbili kwa wimbo wake Aje aliomshirikisha rapper wa Nigeria, M.I Ibaga, ambazo ni Best African Colloboration na Best artist or group in African RnB and Soul.

“Thank you Africa! You made it possible to win two awards @afrimawards. Fans across the world Asanteni sana,” ameandika Kiba.

Naye ameshinda kipengele cha Best Female Artist in Eastern Africa.

“Mungu wetu ni mkubwa sana matendo yake ni ya ajabu sana,” ameandika Nandy kwenye Instagram. “Asante media zote kwa support hii ni nguvu yenu na kiukwel nimeiona familia yangu mpo na mimi sambamba nawapenda sana, menegment yangu mna fanya kazi kubwa sana asanteni kwa uongozi mwema, ma fans wangu nyie ndo kila kitu kwangu nawashukuru kwaku vote mbarikiwe sana ๐Ÿ’™ imerudi nyumbani ๐Ÿ™๐Ÿผ.”

Comments

comments

You may also like ...